C8. DENTAL HEALTH TIPS FROM A DENTIST-OVERCOMING DENTAL CARIES || AFYA YA KINYWA-ZIJUE ATHARI UNAZOWEZA KUZIPATA KWA KUCHELEWA KULITIBU JINO LILILOTOBOKA/KUOZA.
Na Mwandishi Arnold Lusingo (Mwandishi ni mwanafunzi wa udaktari wa afya ya kinywa katika Chuo cha Primary health care Institute, Iringa Contacts: Twitter@kakadentine, FB: Arnold Lusingo)
Ø Jino lililooza au kutoboka ni jino gani?
Ni jino ambalo limepoteza madini yake na kuwa na tundu
katika sehemu moja au zaidi ya jino ambayo hii husababishwa na kazi inayofanywa
na bakteria (fukuo) kutengeza asidi(tindikali).
Kwa jina la kitabibu kutoboka au kuoza kwa jino huitwa
Dental Caries.
Ø Ni
nini hasa visababishi vya jino kutoboka/kuoza?
Ili jino lifikie hatua za mwanzo za kutoboka/kuoza kuna mambo manne ambayo ni lazima yawepo ili jino lioze au kutoboka na mambo hayo ni kama ifuatavyo;
§ Uwepo wa jino(host)
Ni lazima kuwepo na jino litakalo tunza mabaki ya chakula ambacho kina asili ya wanga(sukari)
§ Chakula chenye asili ya wanga.
Pia ni lazima kuwepo na chakula chenye asili ya wanga ambacho hiki huweza kuchachishwa na kugeuzwa kuwa asidi au tindikali ambayo italiharibu jino.
§ Uwepo wa fukuo au bakteria.
Katika mazingira ya uharibifu wa jino ni lazima pia kuwe na bakteria au fukuo watakaochachisha chakula chenye asili ya wanga mna kutengeneza asidi ambayo kitaalamun huitwa Lactic acid, ambapo hii huwa sababu ya uharibifu wa jino.
§ Muda
Kitu kingine hapa ni swala la muda, baada ya chunguzi kadhaa za kitaalamu husema kwamba inachukua muda wa miezi 6-18 mpaka kufikia wakati wa jino kuanza kutoboka au kuoza. Muda wa mabaki ya chakula kukaa mdomoni unapozidi kupungua ndivyo kazi ya bacteria kuharibu meno inapozidi kupungua na kinyume chake.
Ø Ni
kwanini watu wengi huchelewa kulitibu jino mpaka kufikia hatua mbaya za
uharibifu wa jino?
Imeonekana kwamba watu wengi hupenda kukaa na meno au jino lililotoboka kwa muda mrefu bila kulipa matibabu stahiki kwa muda, ni kwasababu;
§ Hatua za mwanzo za mchakato wa uharibifu wa jino huwa hazihusishi maumivu kwenye jino husika.
§ Hata likifikia hatua za maumivu huwa wanatumia dawa za maumivu
§ Wengine hutumia dawa za mitishamba.
§ Hawafanyi uchunguzi wa afya ya kinywa na meno yao.
Ø Je
ni kweli kwamba dawa za mitishamba na za maumivu huweza kuzuia jino kuendelea kutoboka?
Hakuna ukweli wowote kwamba dawa za mitishamba na dawa
za maumivu huweza kuzuia jino kuendelea kutoboka mpaka kufikia hali mbaya.
Ila ni kweli kwamba dawa za mitishamba na za maumivu
huweza kuzuia maumivu ya jino kwa muda, yumkini hata muda mrefu.Ila dawa hizo
haziwezi kuizuia kazi endelevu ya bakteria ya kutengeneza tindikali inayotoboa
jino
Hivyo basi bakteria huendelea na kazi yao ya uharibifu
ambayo kwa wakati huu baada ya matumizi ya dawa zilizoondoa maumivu basi
huifanya kazi hiyo bila mhusika kusikia maumivu makali.
Kazi hii endelevu huendelea mpaka itakapofika wakati
imefika kwenye mzizi wa jino.
Ø Mzizi
wa jino ni sehemu gani hiyo?
kwa kawaida jino limegawanyika katika sehemu nyingi
zikiwa na kazi tofautitofauti, lakini tukilitazama jino kwa nje tunaweza
kuligwanya katika sehemu kuu mbili ambazo ni kichwa(crown) ambayo ni sehemu
inaonekana kwenye kinywa na mzizi wa jino(root) ambayo ni sehemu iliyofunikwa
na fizi hivyo kwa kinywani haiwezi kuonekana, kama ilivyooneshwa kwenye picha
namba 1. Hapa chini
| Picha namba 1. Mzizi wa jino(tooth root) |
Ndani ya mzizi wa jino huwa kuna njia ambayo hupitiwa na mishipa ya damu na neva ambazo ndizo hulipa jino uhai.
Sehemu hii ya mzizi wa jino ikifikiwa na acidi
zinazoharibu jino huwa na maumivu makali sana. Na kufikia huku kuna mambo
kadhaa yanaweza kumpata mhanga wa tatizo hili kama hakufanya matibabu ya jino
kabla ya kufikia hatua hii.
Ø Je
ni athari gani mtu anaweza kuzipata kama hatapata matibabu ya jino lililotoboka
katika hatua za mwanzo?
Zipo athari kadhaa anazoweza kuzipata mtu kama hatapata matibabu ya jino katika hatua za awali za kutoboka kwa meno yake, athari hizo ni kama ifuatavyo;
§ Maumivu makali ya jino.
§ Kufa kwa mzizi wa jino.
§ Jipu kuzunguka mzizi wa jino.
§ Jipu sehemu za kinywa.
§ Matatizo kwenye mfupa wa taya.
1.
Maumivu makali ya jino (pulpitis)
Tindikali inayotengenezwa na fukuo ikiachwa mpaka
ikafikia hatua ya kuufikia mzizi wa jino, huweza kuleta matatizo kadhaa katika
mzizi wa jino ambayo kwa kitaalamu huitwa Pulp
inflammation. Ambayo huwa na dalili kuu ya maumivu makali ya jino hasa
wakati wa usiku, na maumivu haya huweza kufikia kiwango ambacho hayatulii kwa
dawa za kawaida za kuzuia maumivu. Wengi wa watu husubiri dalili hii ndipo
wanakuja hospitali au klinic ya kinywa na meno kwa huduma.
2. Kufa kwa
mzizi wa jino (tooth necrosis)
Picha 2: kuonesha jino lililokufa(lililobadilika rangi) |
Kufa kwa mzizi wa jino, ni hatua nyingine mbaya ambapo
jino linapoteza uhai tena, kwani kiin cha uhai wa jino kipo katika mzizi wa
jino hivyo kama mzizi utakufa maana yake jino limekufa. Dalili zake ni hizi
jino linapoteza uwezo wa kusikia maumivu kabisa, jino linabadilika rangi na
kuwa jeusi au la kahawia nyeusi. Ila huweza kusababisha matatizo katika kinywa
ikiwemo jipu la jino, kama jino hilo halitafanyiwa matibabu stahiki.
3.
Jipu
kuzunguka mzizi wa jino
Picha 2: kuonesha jipu kuzunguka mzizi wa jino |
Uwepo wa fukuo katika mzizi wa jino huweza kupelekea
infections ambazo huweza kusababisha mikusanyiko ya usaha kuzunguka mzizi wa
jino amabayo hii, huwa na dalili zifuatazo, maumivu ya jino, maumivu makali
wakati wa kutafuna, maumivu jino husika likiguswa na mtu husikia kama jino
limezidi urefu meno mengine.
4. Jipu la
kinywa
Picha 4: kuonyesha uvimbe uliotokana na jipu la kinywa |
Jipu lililotokana na jino linaweza kusogea sehemu
yoyote ya kinywa ikiwemo shavuni lakini Zaidi huweza fika hata shingoni na
kichwani. Likifika shingoni huweza kusababisha uvimbe pande zote mbili za
shingo na uvimbe huo unaweza kumzuia mgonjwa kupuma hata kumpelekea kifo kama
hatapata matibabu ya dharura ndani ya muda mfupi. Lakini pia likienda kichwani
hujweza kusababisha jipu la ubongo ambapo pia hii huweza kupelekea kifo
5. Matatizo
kwenye mfupa wa taya. (osteomyelitis)
Jipu haliishii kuleta uharibifu kwenye tishu laini tu
pia huweza kuleta infections mpaka kwenye mfupa wa taya, hii nayo pia huwa na
maumivu makali, uvimbe kwenye taya na hata pia kusababisha usaha kwenye mfupa
wa taya.
Mwisho, napenda nikushauri ya kuwa kutoa meno sio
matibabu mazuri sana kwa kinywa chako, na wala haishauriwi sana ila
kinachofanya matibabu hayo yawepo ni kasumba(mazoea) ya watu kuchelewa kupata
matibabu ya kinywa hivyo, meno kufikia hatua mbaya ya uharibifu kiasi kwamba
matibabu pekee kwa muda huo inakuwa ni kuyatoa tu. Vitu viwili vya kuzingatia,
1.Uonapo dalili yoyote ya jino kuharibika wahi amapema kufika kituo cha afya
wanapotoa huduma ya matibabu ya kinywa na meno ili kupata huduma.
2 Uwe na ratiba
ya kufanya uchunguzi wa kinywa walau mara mbili kwa mwaka.
Mwisho, rafiki nikutakie Afya njema katika utunzaji wa
kinywa chako na hakika tunza kinywa kikutunze.
Comments
Post a Comment