C2: MATUMIZI HATARISHI YA MADAWA NA NAMNA YA MASAHIHISHO YAKE KWA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA KWA AFYA BORA

 


Habari rafiki katika darasa huru,

Ni siku nyingine katika hatua kuwa bora .

Hii Makala ni sehemu ya hotuba yangu kwa jumuiya ya watanzania waishio China (TASAFIC) na jumuiya ya waafrika waishio china (ADiCNET).

Msukumo wa kuandaa mada hii si kwa sababu mimi ni mwanafunzi wa elimu ya madawa bali ni namna ambavyo kwa kiasi kikubwa jamii inayatumia madawa bila kutambua na kuleta madhara ya kiafya kwa mtu binafsi na jamii kwa ujumla. Kwa mfano, katikati ya mwaka 2016 nilipata kutembelea mkoa wa kigoma ambapo mimi si mwenyeji wa mkoa huu hivyo nilipata rafiki ambaye alinihifadhi. Kitu ambacho kinanikumbusha rafiki huyu licha ya soga za hapa na pale ni namna ambavyo aliniambia namna mbayo anatumia madawa kwa ajili ya kupona haraka, alinimbia yeye hutumia dozi mara tatu Zaidi ya daktiari alivyomwambia, kama ni vidonge viwili yeyey hutumia vidonge sita, hii ni miongoni mwa tabia hatari za matumizi ya madawa ambazo tutazijadili kwa kina na namna ya kutumia kwa usahihi kwa usalama na afya yetu. ENGLISH VERSION OF THIS ARTICLE

Kwa muhtasari, Makala hii tuta angazia kwa nini tunahitaji kutumia madawa kwa usahihi, tutajifunza mambo ya msingi namna dawa na mwili hufanya kazi hii itasadia kujenga uelewa kwa nini matumizi Fulani ya dawa ni hatari kwa mwili, mwishoni tutamalizia na kuona matumizi hatarishi na namna ya kuyarekebisha pamoja na vitu vya msingi ambavyo mgonjwa anapaswa azungumze na tabibu au mfamasia wake kabla ya kuandikiwa au kuchukua dawa.

Baadhi ya madawa tutumiayo (Image source: pharmacetia)


1.      UMUHIMU WA KUTUMIA MADAWA KWA USAHIHI KWA AFYA BORA

Tunatumia madawa kutibu magonjwa ili mwili uwe imara hii hutufanya tushiriki shughuli za uzalishajii mali na kijamii kiukamilifu. Madawa si chakula bali ni kemikli ambazo zinasaidia kupambana na hali ya udhaifu wa mwili. Kemikali hizi zisipotumiwa vizuri au kwa uangalifu zinapelekea kudhoofisha mwili na wakati mwingine kumekuwepo taarifa za madhira mabaya kama vifo au ulemevu wa kudumu. Hivyo madawa yapaswa kutumiwa kwa uangalifu.

Kiufupi sana, madawa hutibu kwa aina mbili kuu, aidha kwa kuua vimelea visababisavyo maradhi au kurekebisha mfumo wa seli ambao unafanya kazi isivyostahili na kusababisha mwili kutofanya kazi yake kikamilifu.

Umuhimu wa pili wa matumizi sahihi ya mwadawa ni kujenga jamii yenye afya kwa kujikinga na janga la usugu wa vimelea visababishavyo maradhi. Madawa ya kuua vimelea yasipotumika vyema hupelekea vijidudu hivyo kupata usugu kupelekea athari za kutokupona, kutumia gharama kubwa katika kutafuta madawa bora au mbaya Zaidi kutumia kiwango kikubwa cha dawa kutibu ugonjwa mbao ulikuwa unatibiwa na kiwango kidogo cha dawa. kiwango kikubwa cha dawa hudhoofisha mwili kutokana na mzigo ambao mwili kuzidiwa kuliko kiwango ambacho mwili huweza kuchakata dawa. 

2.      MAMBO YA MSINGI KUFAHAMU KUHUSU MADAWA NA MWILI NAMNA AMBAVYO HUFANYA KAZI KWA PAMOJA. 

(i)              Madawa ni kemikali ambazo huwa na usumu ndani yake.

Kama ambavyo waswahili husema kuwa hakuna mazuri yasiyo na kasoro ndivyo na madawa pia. Madawa ni kemikali ambazo zimefanyiwa utafiti na kuonyesha kuwa zina faida katika kutibu ugonjwa Fulani, baada ya tafiti hizo huruhusiwa kwa matumizi ya binadamu hasa baada ya kuonyesha faida yake ni kubwa kuliko hasara. Hivyo basi, kila dawa ina usumu ambao umekubalika kuwa unaweza kuhimiliwa na mwili wa mwanadamu au faida ya kutumia dawa licha ya kuwa na hasara, faida yake ni kubwa kuliko hasara, hii ni kusema kuwa dawa sis alama katika muda wote kwa matumizi yeyote, hivyo ni muhimu kufuata matumizi bora kama ambayo inapenndekezwa na watengeneza madawa bila kusahau wataalamu wa afya kwa pamoja.

 (ii)            Kunywa dawa sahihi kwa ugonjwa sahihi sio tiba, kunywa dawa sio sumu bali ni dozi ndio huamua kuwa dawa ni dozi au sumu.

Kunywa dawa sahihi kwa ugonjwa sahihi haitoshi kuponya mwili dhidi ya ugonjwa ni mpaka kiwango cha dozi sahihi ya dawa ambayo mgonjwa ameandikiwa. Kisayansi kila dawa ina kiwango chake ambacho sahihi kinachotakiwa kuwa katika mwili ili kupata faida za kimatibabu (therapeutic range), chini ya kiwangi hiki hakuna faida za kimatibabu na Zaidi ya kiwango hiki hupelekea usumu yawa dawa mwilini. 

Usumu wa dawa kwa kuzidisha dozi ya dawa

Madawa licha ya kuwa ni kemikali tofauti tofauti yote huwa na usumu, hivyo basi dawa ikizidi kiwango ambacho huhitajika kimatibabu (therapeutic range) huzalisha usumu kwa kuwa viungo muhimu katika kusafisha taka mwilini yaani figo na ini huzidiwa uwezo, kwa kuwa dawa sumu hivyo hujaa mwilini kuliko kiwango chenye faida ya kimatibabu hivyo kusababisha kutokea kwa usumu ambao huonekana kupitia dalili nyepesi kama kukosa nguvu hadi dalili mbaya kama mtu kuzirai au ulemavu wa kudumu kama ukichaa au upofu.

Je kutumia dawa chini ya kiwango ambacho dozi imependekezwa kuna madhara kwa mwili?

Mgonjwa huandikiwa dozi ya dawa ambayo imekadiriwa kiasi kwamba huua vimelea vyote visababishavyo magonjwa, hivyo dozi inapokuwa chini ya kiwango hupelekea baadhi ya vimelea kusalimika lakini kusalimika huko huja na funzo hasa katika mfumo wa kinga wao kuwa imara Zaidi na kuwa sugu dhidi ya dawa iliyotumika.

Hivyo basi ni muhimu sana kutumia dozi sahihi kwa wakati sahihi kama ambavyo mgonjwa ameshauliwa na wataalamu wa afya.

(iii)          Umuhimu wa ini na figo katika kuchakata na kusafisha mwili dhidi ya usumu wa madawa.

Mtu huweza kuuliza ni nini hatma ya madawa baada ya kumeza? je dawa huwa sehemu ya mwili kama ambavyo huwa tunakula chakula? Majibu ya maswali ni kuwa sehemu kubwa ya madawa takribani 98% huchakatwa na kutolewa nje ya mwili.

Ini (liver) ni kiungo ambacho kina kazi maalum ya kuvunja na kuchakata kemikali hatari zote ziathirizo mwili. Kwa namna ya kipekee sana mwili wa mwanadamu umeumbwa kiasi kwamba chakula chochote kipitiacho tumboni hufyonzwa na lazima kipitie katika ini, baada ya hapo kama kuna sumu kwenye chakula huharibiwa hapo kabla ya kuendelea na safari katika mfumo wa damu. Figo kwa upande wake ni kiungo muhimu katika kusafisha mwili kwa kufanya kama chujio, ambapo taka zisizo hitajika mwili hutolewa kwa njia ya mkojo, asimia 97 ya dawa mabazo hupita katika damu huondolwa kupitia figo. 

(iv)           Dawa huingiliana na dawa, pia dawa huingiliana na chakula au pombe kuleta matokeo yasitorajiwa.

Yawezekana ushawahi kusikia dawa A huingiliana na dawa B, au dawa A haiendani na baadhi ya vyakula kama maziwa au pombe.

Kwa kuwa dawa si shemu ya mwili huwa na namna yake ya kutolewa nje mwili kupitia ini na figo. Pia dawa haikakiwi kuwa juu au chini ya kiwango Fulani katika mwili ili kupata matokeo ya kimatibabu. Hivyo, dawa Zaidi ya mbili zikitumika kwa pamoja huweza kuingiiana katika njia ya kutplewa nje mwili, kuingilina huko hupelekea dawa moja kuchelewa kutolewa mwilini, hivyo kujaa mwilini kuzidi kiwango cha kimatibabu ndipo huleta madhara ya usumu.

Pia baadhi ya dawa zikitumika kwa pamoja huplekea kupunguza ufanisi wa mojawapo, mfanao dawa A kuchochea dawa B kutolewa kwa haraka na mwili, kupelea muda wote dawa B kuwa chini ya kiwango kihitajikacho kwa ajli ya matibabu. 

Muingiliano wa dawa na chakula

Pia baadhi ya vyakula kama juisi, maziwa na pombe huingiliana na dawa, kusababisha aidha usumu wa dawa au kupunguza ufanisi wa dawa.

Mfano, Nifedipine (Procardia) dawa ya kupunguza presha ya juu ya damu ikiingiliana na pombe hufanya pressure ya damu kuwa chini sana, kama ni pombe kali huweza kusababisha pressure ya damu ya mgonjwa kuwa chini matokeo yake ni mgonjwa kukosa fahamu au kupoteza uhai.

Kuna dawa nyingi ziingilianazo na dawa nyingine au na vyakula, hivyo ni vyema Mgojwa kumuuliza mtaalamu wa afya kama dawa husika inaweza tumika na badhi ya vyakula ambavyo mgonjwa hutumia kama pombe, juisi au maziwa.

Baada ya mambo ya msingi kuhusu dawa na mwili tujumuike kuona namna ambavyo watu hutumia madawa hovyo na namna ya kurekebisha kwa kujenga afya bora. 

3.     Matumizi mabya, hatarishi ya dawa na namna ya kusahihisha kwa afya bora.

(i)              Kutokukamilisha dozi ya dawa katika muda husika ulipangwa

Kawaida mgonjwa huandikiwa dozi ya dawa kutumia kwa muda Fulani ikitarajiwa hali itakuwa shwari baada ya kutumia dozi hiyo. Mfano 2x3x7 ikimaanisha vidonge viwili mara tatu kila siku kwa muda wa siku saba. Kutokukamilisha dozi kwa wakati hupelekea usugu kwa vimelea, mbaya Zaidi hupelekea usugu wa ugonjwa hivyo mgonjwa hali hudhorota, hupangiwa madawa ghali na hata kupelekea vifo kwa magonjwa hatarishi yasipodhibitiwa kwa wakati.

Kimsingi, vimelea hupata usugu kwa kuwa si vyote hufa kwa kuwa dozi haikukamilika, hivyo vimelea vichache vilivyobaki hubadilika na kupata usugu ambao hutibiwa kwa dawa nyingine yenye nguvu au kiwango kikubwa cha dawa ya awali. Madhara ya usugu haya mpati mgonjwa pekeyake bali kwa jamii nzima hasa ambapo vimlea vikiambukiwa kwa mtu mwingine, kwa ngazi ya serikali, hupoteza kiasi kikubwa katika kuwekeza shughuli za utafiti katika kutafuta tiba mpya za magonjwa sugu. 

Suluhisho: kutumia dawa ambazo mgonjaamepangiwa kwa wakati, endapo mgonjwa hapati nafuu ni vyema kuasiliana na mtaalamu wa afya aliye karibu na mgonjwa ili kuangalia nmna bora aidha kupewa dozi ya pili au kupangiwa aina nyingine ya matibabu ambayo ni thabiti Zaidi ya awali. 

(ii)            Matumizi ya juu au chini ya kiwango cha dozi kilichopendekezwa

Lama ambavyo imeanishiwa sehemu iliyopita

Matumizi ya dawa kwa kiwango cha juu kuliko dozi iliyopendekezwa na wataalamu wa afya hupelekea usumu kwa mwili kutokana na kupita uwezo wa ini na figo kuweka kuondoa mwilini, hvyo sumu ya dawa huathiri mwili. Matokeo ya kuzidisha dozi ya dawa hujionyesha katika dalili kama kichwa kuuma, kizungu zungu hadi dalili hatarishi kama ulemavu wa kudumu na kifo cha ghafla. 

 SULUHISHO: kutumia dozi sahihi ya dawa husika, hivyo yampasa mgonjwa kuuliza kwa daktari au mfamasia namna ya kutumia dawa husika kabla ya kuchukua dawa kwa ajili ya matumizi.

(iii)          Matumizi ya dawa nyingi kwa wakati mmoja (polypharmacy) kutoka vyanzo tofauti

Tabia ya kutumia dawa nyingi kwa wakati mmoja ambapo mhusika huchukua dawa kutoka chanzo Zaidi ya kimoja pasipo vyanzo hivyo kuwa na taarifa za kuhusu mgonjwa kutumia aina nyingine ya madwa. Dawa huingiliana mwilini hivyo kueplekea kufanya mwili kuwa uwanja wa mapambano na kuleta madhira kwa mwili. 

Licha ya kuwa tabia hii ipo miongoni Zaidi mwa wazee kutokana na hali yao ya mwili kudhoofika na kuathiriwa na magonjwa mengi kwa wakati mmoja, ipo pia mwingoni mwa watu wenye umri rika wa kati. Tabia hii inaweza fanyika kwa kuchangyanya madawa ya hospitalini (dawa za kisasa) na dawa za kienyeji (herbal medicine), inaweza kuwa hatari endapo itafanywa pasipo kuwa na maarifa ya kutosha kujua athari ya dawa husika mabazo muhusika atakuwa anatuamia. 

SULUSHISHO: namna bora ya kutatua hii tabia kwa usalama ni kuwasiliana na mtaalamu wa fya kuwa mgonjwa anatumia dawa nyingine hii itasadia mtaalamu kutoa dawa ambazo ni salama kwa mgonjwa kiasi kwamba hazina muingiliano wenye kuathiri afya ya mgonjwa.

 

(iv)           Matumizi ya madawa yaliyobaki na utunzaji mbovu wa madawa.

Dawa huwa na maelekezo au masharti yake ya kutunzwa ili kududmisha ubora wake kwa matumizi thabiti ya mwanadamu. Matumizi thabiti kwa maana ya usalama. Hivyo dawa inapotunzwa katika mazingira yasiyo kizi viwango hupelekea ubora kupungua au kufanya usumu. Kiufupi, dawa zisipotunzwa katika mazingira bora hupelekea mabadiliko ya kikemkikali kutoka kwenye ubora wake wa awali kuzalisha kemikali nyingine ambazo si dawa tena bali ni sumu. Hivyo ni vyema kutunza dawa katika ubora ambao umependekezwa na wataalamu au wazalishaji. 

4.     Mambo ya muhimu ambayo mgonjwa anapaswa kuyafahamu na kuzungumza na mtabibu kabla ya kutumia dawa.

1.     Mgonjwa ni vyema kuzungumza na daktari dawa ambazo alishawahi kutumia kutibu ugonjwa husika siku za nyuma na ufanisi wake katika kufanya kazi. Hii itamrahisishia mtabibu kutambua dawa ipi itakuwa na ufanisi kwa mgonjwa husika na kuepuka kumpatia madawa ambayo yaweza mletea madhara mgonjwa. Hivyo ni muhimu kutunza kumbukumbu ya madawa ambayo mtu hutumia kwenye daftari maalum.

2.     Mgonjwa ni vyema azungumze na daktari kuhusu kuwa na shida ya viungo muhimu hasa figo na ini, hii itarahisisha kuandikiwa dawa zenye kuendana na hali ya mgonjwa.

3.     Mgonjwa ni lazima amtaarifu daktari juu ya uwepo wa madawa mengine ambayp mgonjwa anatumia (madawa yote hata ya kienyeji), hii husaidia mgonjwa kuandikiwa dawa zisizo na muingiliano na dawa ambazo mgonjwa amekwisha andikiwa tayari.      

4.     Mgonjwa anatakiwa ajue namna sahihi ya kutumia na kuzitunza dawa kwa usahihi dawa. Pia mgonjwa anatakiwa ajue muda ambao anatakiwa atumie dawa kumaliza na kupata nafuu ya kimatibabu. 

6.     Mgonjwa anatakiwa awasiliane na daktari iwapo kuna vyakula au vinywaji kama pombe, soda au juisi ya balungi ambayo haiendani na dawa. 

7.     Mgonjwa anatakiwa ajue dalili ndogo ndogo zisizo rafiki ambazo zinaweza sabababishwa na dawa kama kuhisi uchovu, mwili kuchoka, kichwa kuuma nk. Hii itasaidia kuondoa hofu kwa mgonjwa na hata dalili hizi zinapozidi mgonjwa kujua wapi pa kuanzia.

Rafiki, hongera kwa hatua mbayo umeipiga mpaka hapa, tena hongera sana. Je kuna matumizi mengine ambayo ungependa kujua ni salama au la/ kama ndivo pamoja na maswali, maoni au mchango wowote karibu katika uwanja wa maoni.

Comments

  1. Thanks Mr Masota for a great knowledge that you diligently provide to us.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hello Tenachew team,
      I appreciate your feedback, it is my responsibility to share the knowledge that I have acquired.
      Thanks

      Delete

Post a Comment

Popular posts from this blog

C6: AFYA YA MENO KUTOKA KWA MTAALAMU (DENTAL HEALTH TIPS FROM A DENTIST) || ZIJUE SABABU ZINAZOPELEKEA HARUFU MBAYA YA KINYWA HATA BAADA YA KUPIGA MSWAKI.

C5: NOW YOU KNOW (ABOUT MEDICINE): THE PROPER USES OF CAPSULES

C1. THE CLASS WITHOUT WALLS !